Ticker

6/recent/ticker-posts

Joan Laporta Barcelona 'Haina Mpango Wa Kumuuza' Frenkie de Jong

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Joan Laporta Barcelona 'Haina Mpango Wa Kumuuza' Frenkie de Jong


RAIS Wa Barcelona Joan Laporta amesisitiza kwamba atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha ana mbakiza kiungo Frenkie de Jong Camp Nou na ametanabaisha kwamba Klabu hiyo ‘haina mpango’ wa kumuuza, licha ya kuwa Manchester United ipo katika hatua nzuri ya makubaliano na Barca juu ya kiungo huyo raia wa Uholanzi.

Manchester United waliongeza dau la usajili kwa De Jong mbaka kufikia euro milioni 80 baada ya ofa yao ya mara ya kwanza ya euro milioni 65 kukataliwa, mtandao maarufu kwa habari za michezo wa 90min unadai kwamba chanzo cha kuaminika kinadai kuwa mbaka mwisho wa mwezi june makubaliano yalikuwa yanakwenda vizuri licha ya klabu hizo kuwa katika mvutano juu ya kiasi cha euro milioni 5 kilichopo katika vipengele vya uhamisho wa mchezaji huyo. 

“Nitahakikisha nafanya ntakacho weza kufanya ili kumbakisha Frenkie licha ya kuhitaji kuongezewa nyongeza ya mshahara na tutafanya hivyo,” Laporta alisema hayo wakati akihojiwa kupitia Mundo Deportivo.

Laporta ameongeza kuwa sio Manchester United pekee wanoa muhitaji De Jong zipo timu nyingine zinamuhitaji pia.

“Ni mchezaji wa Barça, na ni moja ya wachezaji wazuri,. Tunajua kuna vilabu vingi vinamuhitaji, Sio Manchester United pekee wanao muhitaji, na hatuna mpango wowote wa kumuuza,” Alisema Rais huyo.

“Tunajua anahitaji kubaki nasi na vigezo vya mchezaji ni vya muhimu sana. Anafuraha kuwepo Barcelona, Ntafanya kila kitu kuhakikisha tunambakiza.

Post a Comment

0 Comments