Ticker

6/recent/ticker-posts

Jack Wilshere Aomba kazi Arsenal

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Jack Wilshere Aomba kazi Arsenal


KIUNGO wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere amefanya mazungumzo na klabu hiyo akitaka kuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana.

Kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 Per Mertesacker anatafuta makocha wa kujaza nafasi mbili baada ya kuondoka kwa Kevin Betsy na Dan Micciche, aliyekuwa kocha wa timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18.

Mwanasoka huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 30 anaamini angali na nguvu za kusakata soka,lakini kulingana na vyombo vya habari jijini hapa, Wilshere amefanya mazungumzo akitaka kuwa kocha msaidizi wa Mertesacker.

Duru za kuaminika zinaeleza kwamba mazungumzo hayo yameanza tu hivi punde.

Wilshere amekuwa bila timu tangu aagane na Aarhus ya Denmark baada ya kuichezea kwa muda mfupi.

“Nimekuwa nikijishughulisha na kazi ya ukufunzi,” alisema kupitia mtandao wa Arsenal.

“Kwa kweli, imekuwa vigumu kujiandaa vyema kama mchezaji, hasa tangu kuzuka kwa Covid-19, na ilibidi niwe nikifanya mazoezi asubuhi katika kikosi kikuu na baadaye kushughulika na masomo ya ukufunzi nyakati za jioni katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 18 pamoja na akina Dan, Max, Chris ambao wamekuwa na msaada mkubwa kwangu.”

“Ninaamini nimepata mafunzo ya kuniwezesha kufaulu kama kocha. Nimejifunza mengi kuhusu ukufunzi, na nimekuwa nikifurahia sana.”

Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal ametumia wakati wake mwingi katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo ulio eneo la Colney siku za karibuni, akijinoa na kikosi kikuu, wakati huo akisaidia timu za wasiozidi umri wa miaka 23 na ile ya wasiozidi umri wa miaka 18, wakati akitafuta timu ya kuchezea.

Post a Comment

0 Comments