Ticker

6/recent/ticker-posts

Isah Ndala Azam Itatikisa sana msimu ujao

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KIUNGO mkabaji wa Azam, Mnigeria Isah Ndala amesema kwa jinsi alivyokiona kikosi cha timu hiyo na mazoezi wanayofanya nchini Misri, anaamini watatikisa sana msimu ujao.

Ndala amejiunga na Azam hivi karibuni akitokea Klabu ya Plateau ya Nigeria akiwa mmoja kati ya viungo wanaotarajiwa kufanya makubwa msimu ujao.

Mchezaji huyo amesema kambi hiyo iliyopo katika Mji wa El Gouna, Misri imewapa utulivu wa kujiandaa vizuri kwa ajili ya Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa na anaamini italeta matunda mazuri.

“Tunaendelea na mazoezi hapa kambini, kila mchezaji anapambana kuhakikisha timu inakuwa imara.

“Nafurahi nimeweza kuzoeana na wenzangu kwa muda mfupi na kadri muda unavyoenda naendelea kuzoea mambo mbalimbali ndani ya timu,” alisema Ndala na kuongeza

“Nafurahia jinsi kila mchezaji anavyojituma mazoezini kwani inaongeza ushindani wa namba kikosini na kuifanya timu kuwa imara.

“Naamini kama haya tunayofundishwa na kuyafanya mazoezini, kila mmoja atayapeleka ndani ya uwanja ligi itakapoanza na hata kwenye mashindano ya kimataifa, basi tutatisha sana msimu ujao,” alisema.

Ndala ambaye pia ni rafiki mkubwa wa kiungo mpya wa Simba, Victor Akpan alisema anaiona Azam ikifanya makubwa msimu ujao ikiwemo hata kutwaa ubingwa.

Post a Comment

0 Comments