Ticker

6/recent/ticker-posts

Injinia Hersi Said Rais wa Kwanza Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Injinia Hersi Rais wa Kwanza Yanga



Injinia Hersi Said amechaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa klabu ya Yanga baada ya kupigiwa kura za ndio.

Hersi amechaguliwa  Jumamosi Julai 9, 2022 kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo alikuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo ya urais.

Mwenyekiti Kamati ya uchaguzi, Wakili Ally Mchungahela amesema kwa mujibu wa ibara ya 23(9) ya kanuni za uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mgombea akiwa mmoja mkutano Mkuu unapitisha azimio la mgombea kuwa Rais.

"Wajumbe mnaridhia Hersi Said kuwa Rais wa Klabu ya Yanga," amesema Mchungahela huku wajumbe wakiitikia ndio.

Mchungahela amerudia mara tatu kauli hiyo wajumbe wakionekana kumkubali.

Baada ya kupiga kura hizo za wazi za ndio Mchungahela amemtangaza rasmi kuwa Rais wa klabu hiyo.

Wajumbe hao walianza kuimba Hersi Hersi ikamlazimu kupanda jukwani na kuwapungia mikono ikiwa ishara ya shukrani kwa kumuamini.

Post a Comment

0 Comments