Ticker

6/recent/ticker-posts

Hukumu Ya Haji Manara Yaleta Taharuki Kwa Wanasheria

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Hukumu Ya Haji Manara  Yaleta Taharuki Kwa Wanasheria

Baada Siku tatu tangu Haji Manara apewe adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili cha kutojihusisha na soka na kulimwa faini ya Sh20 milioni kwa kosa la kumtolea maneno ya ovyo Rais wa Shirikisho la Soka (TFF), suala lake bado limekuwa gumzo na kuzua maswali tata matano.

JE,UNATAFUTA AJIRA? BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI

Wanasheria mbalimbali wamelizungumzia jambo hilo, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, iliyomuadhibu Manara kwa tukio linalodaiwa kutokea katika fainali ya Kombe la ASFC, Julai 2 kati ya Yanga na Coastal Union, Kichere Chacha Waisaka akisema licha msemaji huyo wa Yanga kufungiwa, yupo huru kwenda uwanjani kwenye mechi yoyote kutazama.


“Ni haki yake kikatiba, anaruhusiwa, ambacho amefungiwa ni kushiriki kwenye masuala mengine ya soka, lakini si kwenda kutazama mechi yoyote ile uwanjani, hiyo ni haki yake,” alisema Kichere, wakati Manara katika akaunti yake rasmi ya Instagram ulisomeka ujumbe kuwa; “Sipoi hata tone, tabu ipo palepale, sana sana ndio itazidi, otherwise waje kuniua.” Hata hivyo, Kichere amebainisha kwamba, kama Manara hataridhika na adhabu hiyo ni haki yake kukata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya TFF ndani ya siku 21. Yanga imesisitiza adhabu aliyopewa ni kubwa na klabu inamuunga mkono katika kutafuta haki.


Emmanuel Muga, alisema adhabu ya Manara haikupaswa kupitia kwenye Kamati ya Maadili, akihoji kanuni za TFF kwa kosa kama alilotenda Manara zinamtambua kama ni kiongozi wa Yanga? “Kanuni zinasema kwa viongozi wa soka, swali ni je, Manara ni kiongozi Yanga? Pia adhabu ya Sh20 milioni kwenye kanuni za TFF haipo, labda waibabadilishe hivi karibuni, ningeshauri tu kamati zote za TFF zinapaswa kuwa huru.”


Kasanda Mitungo, mwanasheria wa kujitegemea alisema; “Sikuona sababu ya sekretarieti kushtaki wakati mlalamikaji ambaye ni Karia dhidi ya mlalamikiwa Haji yupo, Sekretarieti ilifanywa nini na Haji hadi kufungua kesi? Katika sheria hakuna mtu anaweza kuwa jaji katika kesi yake mwenyewe, hivyo sekretarieti ambayo inamlalamikia Haji ndiye inaiwezesha Kamati.”

“Ukiachilia mbali fungua shauri, walipaswa kumleta Karia kama shahidi kama wameshindwa kumleta kama mlalamikaji, kwani ni rahisi yeye kutueleza kilichotokea kuliko mwingine yoyote na je mlalamikiwa alitumia lugha gani au ishara gani.

“Tulipaswa tuambiwe kama ni lugha ya mwili tuambiwe ni zipi, lakini kwenye hukumu haikusemwa, zaidi ya hapo hayo ni mashaka na kwenye jinai inapaswa kuthibitisha kesi pasi mashaka yoyote.”

‘’Tungeambiwa Karia pia alitoa maneno gani katika majibizano hayo, lakini pia hatujaambiwa tafsiri ya lugha ta mwili na ‘conduct’ ya rais haikuwa jinai? kwani katika ushahidi hatujaambiwa nani alianza, inawezekana Karia alikuwa akijihami au Haji alikuwa akijihami?. Mjadala wa hukumu ya Manara na Karia umeendelea kuwa gumzo.

Post a Comment

0 Comments