Ticker

6/recent/ticker-posts

George Mpole kutua Simba Muda Wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 George Mpole kutua Simba Muda Wowote



Mshambuliji wa Geita Gold George Mpole baada ya kufunga Mabao 17 kwa msimu huu na kuibuka kinara wa mabao amefunguka na kuweka wazi ishu yake na Simba.

Akihojiwa, Mpole alisema amepokea ofa nyingi kutoka timu za ndani na nje ya nchi zikitaka kumsajili lakini kwa Tanzania Simba ndio wapo katika nafasi nzuri ya kumsajili.

Mazungumzo kati ya Simba na Mpole hayajakamilika kutokana na ofa nyingine kubwa alizokuwa akisikilizia kutoka DR Congo, Uturuki na Morocco lakini nazo hadi sasa hakuna aliposaini.

“Kuna ofa zipo nyingi tu lakini sijasaini popote, nilihitaji kwanza kutimiza malengo ya msimu huu kisha ndiyo hayo mengine yafuate,”alisema.

“Simba ni miongoni mwa timu nilizowasiliana nazo lakini hatujamalizana, naamini siku si nyingi kila kitu kitaenda sawa na mtajua Mpole nitakuwa wapi msimu ujao,” alisema Mpole.

Taarifa za ndani tulizo nazo ni kwamba Mpole msimu ujao atacheza Simba kwani wameshaafikiana mambo mengi na mkataba ni miaka miwili hivyo bado yeye kusaini tu.

Vigogo wa Simba jana walikuwa wakipambana kuhakikisha ishu ya mchezaji huyo inamalizika haraka kwa sababu Azam pia nao wanatajwa kumuwania pamoja na Singida Stars.

Uongozi wa Geita kupitia kwa Katibu mkuu wa Bodi,Zahra Michuzi alieleza kuwa timu hiyo haitakuwa na pingamizi la Mpole kuondoka kikosini hapo kama mwenyewe atahitaji kwenda kutafuta malisho mapya.

“Tumeshafanya naye mazungumzo lakini kama akipata ofa nzuri na akachagua kuondoka basi tutampa baraka zote na tutakachokifanya ni kutafuta mbadala wake. Tuna wachezaji wengi  hivyo akiondoka Mpole mmoja tutaongeza kina Mpole watatu,” alisema Zahra.

Akizungumzia msimu wake, Mpole alisema; “Haikuwa rahisi, msimu ulikuwa mgumu pia kulikuwa na kupanda na kushuka. Lengo kuu ilikuwa kuitumikia timu kuhakikisha tunafika malengo na imekuwa hivyo.”

“Mwanzo sikuwaza kuwa mfungaji bora lakini kadri nilivyozidi kufunga wazo hilo lilinijia na baadae nikazidi kulifanyia kazi na namshukuru Mungu hatimaye imetimia,” alisema Mpole ambapo jana Mayele aliposti kwenye akaunti yake akimpongeza na kumtakia kila la heri.

Post a Comment

0 Comments