Ticker

6/recent/ticker-posts

Gael Bigirimana atambulishwa yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Gael Bigirimana atambulishwa yangaRAIS mpya Yanga, Hersi Said amemtambulisha rasmi kiungo wao mya aliyewahi kucheza Newcastle United ya Uingereza, Gael Bigirimana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere unapofanyika uchaguzi wa timu hiyo.

Akizungumza mbele ya wajumbe, Hersi amesema mchezaji huyo ana sifa kubwa kwani amecheza katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Hersi amesema wao wanasajili wachezaji wazuri na ndio maana wamemchukua mchezaji  wa zamani wa klabu ya Newcastle iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu nchini Uingereza.

“Sisi tunasajili na tumeahidi kabisa kushusha vifaa, huyu hajacheza timu ndogo bali amecheza timu kubwa na kwenye Ligi Kubwa,” amesema Hersi na kuongeza;

“Wanasema eti Mayele ataenda Kaizer Chiefs, sisi wenyewe tunachukua wachezaji kutoka kwao huko.”

"Sijaja kunyonya timu, bali nimekuja kufanya kazi, Naamini nitakuwa nimefungua milango wachezaji wengine wengi wanaocheza Europe kuja kucheza Yanga, Nilipata ofa nyingi Ulaya ila baada ya kuziskiliza Plans za Rais Mpya wa Yanga nikaona ni muda sahihi wa kurudi kucheza Mpira Afrika na Klabu hii Kubwa na yenye historia ya kipekee" @gaelbigiofficial
Tazama hapa video ya Gael Bigirimana akitambulishwa yanga

Gael Bigirimana Akiwa sambamba na rais wa yanga Injinia Hersi


Post a Comment

0 Comments