Ticker

6/recent/ticker-posts

Firmino anahusishwa na Juventus

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KWA mujibu wa Jarida maarufu la michezo la Tuttomercato ni kwamba, ‘Vecchia Signora’ maarufu kama vibibi kizee vya turin au Juventus wanajiandaa kutuma ofa ya euro milioni 23 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino kutoka Brazil.

Roberto Firmino anaweza kuwa mshambuliaji wa pili kuondoka Liverpool baada ya Sadio Mané kuondoka na kuelekea Bayern Munich mapema msimu huu wa majira ya joto. 

Mshambulizi huyo wa Kibrazil, ambaye mwanzoni hakuweza kuguswa na Klopp katika miaka yake ya kwanza Anfield, amekuwa chaguo la pili la Klopp,nyuma ya wachezaji kama Diogo Jota na Luis Díaz. Mkataba wa Mbrazil huyo unatarajiwa kumalizika mwishoni Juni 2023.

Firmino alisajiliwa kwa euro milioni 41 akitokea Hoffenheim ya Ujerumani miaka saba iliyopita.

Mchezaji huyo, kwa upande wake, yuko tayari kwenda mahala pengine ambapo atapata uhakika zaidi wa kucheza katika kikosi cha kwanza kama ilivyoripotiwa na Tuttomercato.

Bianconeri wapo sokoni wanatafuta mshambuliaji nambari ‘9′ mwenye uwezo wa kucheza na Dusan Vlahovic, licha ya kwamba Mserbia huyo kasha jiakikishia namba katika kikosi cha kwanza. Morata anaonekana kuelekea Atlético Madrid, na kuwafanya Juve kuingia sokoni kwa ajili ya kumtafuta mshambuliaji mwingine.

Post a Comment

0 Comments