Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Chelsea wana matumaini watawashinda Bayern Munich katika mbio za kumsajili Matthijs de Ligt kutoka Juventus, licha ya muholanzi huyo kufanya ' mazungumzo ya awali ' na mabingwa hao wa Ujerumani.

Chelsea wanataka mbaka kufikia mwishoni mwa wiki wawe wamekamilisha usajili wa mchezaji mmoja wapo kati ya De Ligt au Nathan Ake wa Manchester City .

Kocha Mpya wa Paris Saint-Germain  Christophe Galtier ameweka wazi nia yake kwamba anapenda kuona Neymar anabakia kikosini hapo, Ingawa taarifa za hivi karibuni zanadai mabigwa hao wa Ufaransa wanampango wa kuachana na Mbrazili huyo.

Juventus wakati wowote watakamilisha usajili huru wa viungo Paul Pogba na Angel Di Maria baadae wiki hii baada ya wachezaji hao kufudhu vipimo vya Afya.

Kwingineko, mshambuliaji wa zamani wa Juve Paulo Dybala yupo katika hatua za mwisho kujiunga na Inter, licha ya Nerazzurri kushindwa kutangaza usajili wa nyota huyo wakisubili kuuza baadhi ya wachezaji wao ili kupata kitita cha kumsajili mchezaji huyo. Beki wa Torino Gleison Bremer anajiandaa kutua San Siro.


Post a Comment

0 Comments