Ticker

6/recent/ticker-posts

Erik ten Hag awataka vijana wa Man Utd kujituma kama wanataka nafasi kikosi cha kwanza

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Erik ten Hag awataka vijana wa Man Utd kujituma kama wanataka nafasi kikosi cha kwanza


Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ametoa wito kwa wachezaji chipukizi waliopewa nafasi kwenye kikosi chake kilichopo ziarani nchini Thailand  kabla ya msimu mpya kuanza ‘kuonyesha’ uwezo ili waweze kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

Ten Hag amechagua chipukizi kadhaa kwa ajili ya safari hiyo inayoanzia nchini Thailand kabla ya kuhamia Australia.Chipukizi walio chaguliwa kwa ajili ya maadalizi ya msimu mpya ni pamoja na magwiji wa Argentina, Alejandro Garnacho, Hannibal Mejbri, Charlie Savage, Zidane Iqbal, James Garner na wengineo.

Kocha huyo wa Uholanzi ana sifa ya kukuza vipaji, akiwa amejenga msingi wa timu yake ya Ajax ambayo ilitinga fainali ya Ligi ya Mabingwa 2019 akiwa na wachezaji wa nyumbani.

Kuna uwezekano wa kuwa na nafasi kubwa kwa Chipukizi wa United kucheza katika mechi zijazo za kirafiki kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Liverpool, Melbourne Victory, Crystal Palace na Aston Villa, lakini ikiwa tu watathibitisha Ubora wao kwa Ten Hag.

"Ninachotaka kuona ni wanajifunza lakini pia wanaonyesha uwezo wao kwa sababu wanapaswa kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza," bosi huyo aliiambia ManUtd.com.

“Lazima utetee nafasi yako. Ina maana unapaswa kujituma kila siku, ambapo inahitajika mtindo fulani, njia fulani ya maisha ambayo wanapaswa kukabiliana nayo, ambayo labda hawajui bado. Lakini ninatazamia sana kuona ikiwa wanaweza kuifanya.

"Natumai mmoja au wawili, wanaweza kujituma na kuingia kwenye kikosi lakini, kama wanataka kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo, wanapaswa kufanya hiyo." 

Post a Comment

0 Comments