Ticker

6/recent/ticker-posts

Cristiano Ronaldo akataa ofa ya mkataba wa €275m kutoka Saudi Arabia

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Cristiano Ronaldo akataa ofa ya mkataba wa €275m kutoka Saudi Arabia

Cristiano Ronaldo amekataa ofa ya kandarasi kubwa yenye thamani ya €275m kutoka kwa klabu ambayo jina lake halija faamika kutoka nchini Saudi Arabia.

Ronaldo amekuwa akihusishwa sana na kutaka kuondoka Manchester United msimu huu wa majira ya joto, huku Chelsea wakipewa nafasi kubwa ya kumsajili fowadi huyo.

Siku ya Alhamisi The Blues walitoa taarifa kwamba wameamua kumfuatilia CR7 - licha ya mmiliki mpya Todd Boehly kuvutiwa na fursa ya uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ESPN, klabu iliyo onyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or ni klabu ambayo haijafahamika kutoka nchini Saudi Arabia. Klabu hiyo inasemekana Ilikuwa tayari kuwasilisha dau la €30m kwa ajili ya kupata huduma ya Ronaldo, na pia kumpa mchezaji huyo mkataba mnono ambao ungemfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kulipwa Mshahara wa €275m kwa miaka miwili.

Ronaldo amekataa Ofa hiyo, hata hivyo Inaonekana kuna uwezekano mkubwa Akasalia Manchester United baada ya dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi.

Mshambulizi huyo alijiunga tena na Mashetani Wekundu msimu uliopita wa majira ya joto, na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 24 katika mashindano yote msimu wa 2021/22, klabu hiyo ilipambana na kufanikiwa kumaliza nafasi ya sita kwenye Ligi - imefunga mabao 57 pekee katika michezo 38 ya ligi.

Man Utd wanaonekana kuwa na matumaini zaidi kwa msimu ujao,baada ya kumteua Erik ten Hag kuwa meneja wao mpya.

Post a Comment

0 Comments