Ticker

6/recent/ticker-posts

Man Utd Wakaribia Kumsajili Christian Eriksen

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Man Utd Wakaribia Kumsajili Christian Eriksen


Manchester United wanauhakika watashinda mbio za kumsajili kiungo Christian Eriksen baada ya mkataba wake na Klabu ya Brentford kumalizika.

Eriksen Alisajiliwa na Brentford kwa mkataba wa miezi sita tangu mwezi January na kuisaidia timu hiyo kusalia Ligi kuu  nchini Uingereza maarufu kama  Premier League.

Eriksen Aliwaambia Brentford anahitaji kuondoka tangu mwezi ulio pita. Klabu yake ya zamani ya Tottenham pia inaangalia uwezekano wa kumrudisha kiungo huyo licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa virabu kadhaa ambavyo vimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya kiungo huyo,. Crystal Palace, Newcastle na West Ham vyote vinamuhitaji.

Manchester United wanauwakika wa kumsajili kiungo huyo mwenye miaka 30 baada ya mazungumzo na kiungo huyo kwenda vizuri wikiendi. 

Erik ten Hag's amekuwa msaada mkubwa kuhakikisha Eriksen anajiunga nao, na Eriksen amevutiwa pia na mipango ya usajili ya Manchester United kwa msimu huu na kwa hapo baadae.

Manchester United tangu muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na Eriksen, Ambae aligoma kutua Old Trafford mwaka 2019 kwajili ya mapenzi yake kwa Spurs. 

Kwingineko United, wanaendelea na mazungumzo na kiungo Frenkie de Jong wa Barcelona, huku beki wa kushoto wa  Feyenoord Tyrell Malacia akiwa anasubilia vipimo vya Afya ili aweze kujiunga na United.


Post a Comment

0 Comments