Ticker

6/recent/ticker-posts

Christian Eriksen atua Manchester United

Manchester United kupitia website yao wamethibitisha kukamilisha Usajili wa mchezaji Christian Eriksen kwa mkataba wa miaka mitatu.

Christian Eriksen amejiunga na United kama mchezaji huru akitokea Brentford baada ya mkataba wake wa miezi sita kuisha.


Mchezaji huyo mwenye miaka 30 amechagua kuendelea kucheza soka Old Trafford baada ya kurejea vyema katika kiwango chake akiwa na Brentford msimu uliopita - alijiunga na Bees miezi saba baada ya kupata mshtuko wa moyo alipokuwa akiichezea Denmark katika michuano ya Euro 2020.

Eriksen amecheza michezo 237 ya Premier League, akifunga mabao 52 na kutoa pasi 66 za mabao. Bado ni moja ya wachezaji bora zaidi duniani, na ataongeza ubora zaidi kwenye safu ya kiungo ya United baada ya kuondoka kwa Paul Pogba msimu huu wa majira joto.

Ni mchezaji wa pili kusajiliwa na United msimu wa huu wa majira ya joto, baada ya Tyrell Malacia kuwasili kutoka Feyenoord, United wanatarajia kutangaza sajili nyingine wiki zijazo. Frenkie de Jong ndiye mlengwa namba moja katika safu ya kiungo, huku dili la nyota wa Ajax Lisandro Martinez likikaribia kukamilika siku za hivi karibuni.

Eriksen hatoweza kujiunga na ziara ya United huko Australia hivyo atakutana na wachezaji wenzake watakaporejea Carrington. 

Post a Comment

0 Comments