Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea wathibitisha kumsajili Raheem Sterling kutoka Man City

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Chelsea wathibitisha kumsajili Raheem Sterling kutoka Man City


Chelsea wamekamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Uingereza Raheem Sterling kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Manchester City.


Chelsea wamekubali kulipa takriban £50m kama ada ya uwamisho kwa ​​wapinzani wao wa Premier League, Sterling ameondoka Etihad baada misimu saba ya mafanikio akifanikiwa kubeba makombe akiwa na City.


Baada ya kufanyiwa vipimo vya Afya mjini London, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesafiri kuelekea Florida kujiunga na wenzake kwajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani siku ya Jumanne kabla ya kutambulishwa kama mchezaji wa Chelsea.


Sterling alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na City na alionyesha nia ya kutaka kupata changamoto mpya sehemu nyingine.


Akiongea na tovuti rasmi ya Chelsea, Sterling alisema kuwa alifurahishwa kurudi London: 'Ni wazi nimepata mafanikio mengi katika kazi yangu hadi sasa, lakini bado kuna mengi zaidi ya kufikia na ninasubiri kwa hamu kufanya hivyo.


"London ni nyumbani kwangu ambapo mambo yangu yote yameanzia, inafurahisha kuwa sasa nina nafasi ya kucheza mbele ya marafiki na familia. Ninatazamia kukutana na mashabiki hivi karibuni. .


"Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Todd, Behdad, Thomas, na wote waliohusika katika kufanikisha mchakato wa kunifikisha hapa."


Sterling anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Stamford Bridge katika utawala wa mmiliki mpya bwana Todd Boehly , mmiliki mpya analenga kuimarisha safu ya ulinzi kwa kuwaongeza Nathan Ake na Kalidou Koulibaly wa Napoli.


Chelsea wanatafuta nyongeza ya mshambuliaji, kufuatia Romelu Lukaku kurejea Inter kwa mkopo - Raphinha anakaribia kujiunga na Barcelona. Ousmane Dembele ne anakaribia kuongeza mkataba ili kusalia Camp Nou.


Chelsea wanaelekeza mawazo yao kwa Mshambuliaji Antony wa Ajax na Serge Gnabry wa Bayern Munich, huku Rafael Leao wa Milan pia akibaki kwenye rada zao.

Post a Comment

0 Comments