Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Yaachana na Deus Kaseke

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 𝗔𝗦𝗔𝗡𝗧𝗘 𝗗𝗘𝗨𝗦 𝗞𝗔𝗦𝗘𝗞𝗘

  • Umekuwa sehemu kubwa ya mchango wa mafanikio kwenye Klabu yetu, Tunakutakia kila la kheri na mafanikio uendako. 

𝗢𝗻𝗰𝗲 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝗻𝗰𝗵𝗶, 𝗔𝗹𝘄𝗮𝘆𝘀 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝗻𝗰𝗵𝗶


KLABU ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na kiungo wake, Deus Kaseke baada ya mkataba wake na timu hiyo kuisha msimu huu.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2015 ameshindwa kuongezewa mkataba mpya kutokana na kushindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara chini ya Kocha Nasreddine Nabi huku akitumika zaidi wakati akitokea benchi.

Awali ilielezwa utitiri wa viungo wengi wa pembeni kwenye timu hiyo wakiwemo, Farid Mussa, Jesus Moloko, Chico Ushindi, Denis Nkane, Dickson Ambundo na wengine wapya waliosajiliwa kama Aziz KI na Bernard Morrison ndio sababu kubwa ya yeye kuachwa.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram baada ya kuachwa Kaseke aliandika; "Asanteni sana Yanga, mmekuwa sehemu kubwa saana ya maisha yangu ya mpira, nashukuru kwa sapoti kubwa mlionipa kipindi chote nilichotumikia timu ya Wananchi."

Kaseke ambaye ameitumikia Mbeya City na Singida United kabla ya kurejea tena Yanga inaelezwa amemalizana na wageni wapya wa Ligi Kuu Bara, Singinda Big Stars ili kuwatumikia msimu ujao.


Post a Comment

0 Comments