Ticker

6/recent/ticker-posts

Nasreddine Nabi aonya mastaa Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Kocha Mkuu wa Yanga  Nasreddine Nabi, amefurahia usajili uliofanywa na uongozi mpaka sasa lakini akaahidi kutakuwa na mabadiliko makubwa kikosini na amewatumia salamu wachezaji huko walipo.

Alichosema Nabi nikwamba usajili umekamilika kwa asilimia 100 wakiwapata mastaa wao wote kama ambavyo waliwahitaji tayari kwa msimu mpya.

Nabi aliongeza kuwa ujio wa mastaa hao watano wapya wa kigeni utabadilisha sura nzima ya kikosi chao cha msimu ujao na ufanisi utakuwa mkubwa zaidi.

"Nawapongeza viongozi wangu lakini pia mfadhili wetu Ghalib (Said Mohammed), tulichopanga kutafuta tumekipata kama tulivyohitaji, hii ni hatua kubwa muhimu," alisema Nabi.

"Tumewapata wachezaji watano ambao hawa sasa ni mahitaji halisi ambayo tuliyahitaji, tunatarajia makubwa kutoka kwao ukiongeza na hawa waliopo.

"Ujio wa hawa kwanza tunaweza kusema tutakuwa na timu bora zaidi lakini mapema niseme kitu kwa wachezaji wangu,kila mmoja anatakiwa kupumzika lakini akijiandaa kiakili tunaweza kuwa na mabadiliko makubwa ya timu hii,"alisema na kuongeza kwamba Bernard Morrison amempa maelekezo ya jinsi ya kujiweka fiti zaidi kwavile yeye alipumzika muda mrefu tofauti na wenzake.

Nabi alisema anajua tayari ni mifumo gani atatumia kwa msimu ujao lakini akawataka wachezaji wake hasa walioitumikia Yanga msimu uliopita wajipange kwa ushindani wa nafasi na hakutakuwa na mbadala.

"Haina maana kama ulicheza vizuri msimu uliopita kwamba msimu ujao utakuwa na nafasi ya uhakika lakini pia hata kama umekuja haina maana kwamba utakuwa na nafasi ya kuanza, tunahitaji kuwa na ushindani utakaosaidia timu kushinda,"alisema.

Wapya waliosajiliwa Yanga ni beki Mkongomani, Joyce Lomalisa, viungo Gael Bigirimana na Bernard Morrison Aliye rejea akitokea Simba,washambuliaji ni Lazarous Kambole na Stephan Aziz KI ambaye muda wowote atatambulishwa Yanga.

Post a Comment

0 Comments