Ticker

6/recent/ticker-posts

Mayele apewa jukumu zito

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Nasreddine Nabi  ampa jukumu zito Mayele


Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amempa jukumu zito mshambuliaji wake Fiston Mayele kuhakikisha kuwa anaiongoza timu kutwaa kombe la Shirikisho la Azam.

Nabi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo wa kesho wa fainali ya FA dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Amesema kuwa kwa sasa Mayele amevunjika moyo baada ya kushindwa kutimiza malengo yake ya kuwa mfungaji bora wa Ligi hivyo kukosa kiatu cha dhahabu kilichochukuliwa na Geogre Mpole wa Geita Gold.

"Mayele amevunjika moyo kukosa kiatu cha dhahabu ambacho kilikuwa ni lengo lake kubwa baada ya kufanikisha timu kutwaa ubingwa lakini nimtie moyo kuwa yeye bado ni mchezaji mkubwa tu kiatu atapata wakati mwingine kwa Sasa aweke akilini namna ya kuisaidia timu kuchukua kombe la FA". amesema Nabi

Nabi amesema kuwa kilichomwangusha Mayele katika nafasi hiyo ni majeraha yaliyokuwa yanamsumbua lakini pia mabao yake mawili kukataliwa katika mechi tofauti katika msimu wa Ligi.

Post a Comment

0 Comments