Ticker

6/recent/ticker-posts

Pogba akaribia kutua Juventus

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Paul Pogba kutua Juventus Muda wowote


MKURUGENZI Mtendaji wa Juventus, Maurizio Arrivabene, ameweka wazi urejeo wa kiungo Paul Pogba akitokea Manchester United kuwa unazidi kukaribia, huku mazungumzo ya uhamisho huru yakikaribia kukamilika.

Bado kuna baadhi ya mambo yanahitaji kutatuliwa kabla ya mkataba kukamilika, ikiwa ni pamoja na haki za picha na vipengele vingine vya kibiashara.

Hata hivyo, akizungumza na Tuttosport, Mkurugenzi Mtendaji wa Juventus, Arrivabene ameweka wazi kuwa mazungumzo yalikuwa yanaendelea 'vizuri sana' na kwamba uhamisho huru unapaswa kukamilika mapema Julai hii.

"Tunazungumza naye, mambo yanaendelea vizuri sana," alisema Arrivabene.

"Uwepo wake (Pogba) pia utakuwa wa msingi kutoka kwa mtazamo wa kibiashara, hata kama ndoto yangu ni kuwa na mchezaji wa Kiitaliano ambaye anatambulika kimataifa kama Totti, Del Piero, Buffon."


Post a Comment

0 Comments