Ticker

6/recent/ticker-posts

Mabosi FIFA na UEFA Blatter na Platini Wanusuriwa na Mahakama

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mabosi FIFA na UEFA Blatter na Platini Wanusuriwa na Mahakama 

  • Sepp Blatter na Michel Platini wameondolewa mashtaka katika kesi ya ulaji rushwa na mahakama ya Uswizi.
  • Blatter ni rais wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA huku Platini akiwa bosi wa zamani wa UEFA. 
  • Mahakama ilikataa ombi la upande wa mashtaka lililotaka kifungo cha kuahirishwa cha mwaka mmoja na miezi minane.



Waliokuwa viongozi wakubwa wa soka duniani Sepp Blatter na Michel Platini wameondolewa mashtaka katika kesi ya ulaji rushwa ambayo ilikuwa ikiwakabili. 

Mahakama ya Jinai ya jiji la Bellinzona nchini Uswizi ilitupilia mbali ombi la upande wa mashtaka lililotaka kifungo cha kuahirishwa cha mwaka mmoja na miezi minane kufuatia uchunguzi ulioanza mwaka 2015. 

Blatter, rais wa zamani wa FIFA na mwenzake wa UEFA Platini, walifikishwa mahakamani kwa malipo ya dola milioni 2.05 kwa Platini mwaka 2011. 

Kwa mujibu wa mahakama, mwaka 2011, Platini aliwasilisha kwa FIFA cheti feki cha kudai malipo ya huduma yake kama mshauri wa FIFA kati ya mwaka 1998 na 2002.

Blatter hata hivyo alisisitiza kuwa wawili hao walikuwa wamefanya makubaliano kwa njia ya mdomo kuwa sehemu ya malipo ya Platini ifanywe baadaye, uwezo wa kifedha wa FIFA ukiruhusu. 

Wawili hao walituhumiwa kughushi cheti hicho; Blatter akikabiliwa na makosa ya jinai ya matumizi mabaya ya pesa huku Platini akikabiliwa na makosa ya kuhusika katika mipango ya Blatter.

Wawili hao walisisitiza kuwa hawana makosa wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo kulikofanyika kuanzia Juni 8 hadi Juni 22 na sasa wameondolewa mashtaka. 

Post a Comment

0 Comments