Ticker

6/recent/ticker-posts

BENZEMA: NIMEJIFUNZA KWA RONALDO AKIWA REAL MADRID ILI NIWE BORA

 


Mshambulajii wa Kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema amefichua kwamba alimsoma sana Cristiano Ronaldo huku akitafuta kujifunza kutoka kwa nyota huyo wa Ureno katika klabu ya Real Madrid walipokuwa wakicheza pamoja.

Benzema na Ronaldo walijiunga na timu ya Madrid katika msimu mmoja, huku Benzema akitokea  Lyon na Ronaldo akitokea Manchester United.

Ronaldo aligonga uwanjani Santiago Bernabeu na kuwa nyota mara moja pale Hispania, ingawa ilichukua muda mrefu kidogo kwa Benzema kufikia kiwango chake cha juu.

Lakini imeonekana wazi kwamba notes zimefanya kazi baada ya msimu huu kuondoka na mataji mawili pamoja na kuwa mfungaji bora katika mashindano yote mawili. Na pia ni moja ya wanaohisiwa kuweza kuchukua Ballon d’Or mwaka huu

Post a Comment

0 Comments