Ticker

6/recent/ticker-posts

Bayern Munich Wasisitiza hawana Mpango wa Kumsajili Cristiano Ronaldo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mkurugenzi wa Masuala ya Michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic amesisitiza kwamba klabu hiyo haina mpango wa kumsajili Cristiano Ronaldo katika msimu huu wa majira ya joto, licha ya mshambuliaji wao nyota Robert Lewandowski kukaribia kuondoka.

Taarifa za awali ni kwamba, Ofa ya Barcelona ya €50m Imekubaliwa na Bayern kwa ajili ya Uhamisho wa Lewandowski, huku Barcelona wakitumai uhamisho huo utakuwa Umekamilika kufikia mwishoni mwa juma.


Kuondoka kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland kutaiacha Bayern ikiwa na pengo kubwa katika safu yake ya ushambuliaji, licha ya kumwongeza saido mane kutokea liverpool.

Hata hivyo, kwa mara nyingine, viongozi wa juu wa Bayern wamekataa kabisa mshambuliaji huyo wa Manchester United kujiunga na Bayern  Munich katika msimu huu wa majira ya joto.

"Ninamheshimu sana Cristiano Ronaldo, mafanikio yake na kazi yake. Lakini kwa mara nyingine tena: Hiyo ilikuwa na sio mada kwetu," Salihamidzic aliiambia Sport.

Ronaldo aliwaomba United kuzingatia ofa zozote zinazofaa ili aweze kuhama katika msimu huu wa majira ya joto. Chelsea, Bayern na Napoli wote kwa pamoja wamejitoa katika kinyang'anyiro cha kumuhitaji Mshambuliaji huyo.

Mwisho Kocha wa United Mholanzi Erik ten Hag amesisitiza kwamba bado anamuhitaji Ronaldo katika klabu hiyo msimu huu.

Post a Comment

0 Comments