Ticker

6/recent/ticker-posts

Barcelona wakamilisha usajili wa Raphinha kutoka Leeds United

 Barcelona wamethibitisha kukamilisha Usajili wa Raphinha kutoka Leeds United kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

Miamba hao wa Catalan walitangaza siku ya Jumatano kwamba wameafikiana kila kitu cha msingi na, baada ya kufaulu vipimo vya afya, Raphinha atasaini mkataba na Barcelona kabla ya kutambulishwa siku ya Ijumaa alasiri.


"Ndoto yangu ya utotoni Imetimia kwangu na kwa familia yangu," Raphinha alisema wakati Akijiunga na Barca. "Nitajitolea kwa uwezo wangu wote kuisaidia timu."

Katika taarifa ya kuagwa kwake kwenye tovuti ya klabu, Leeds wamesema: "Tunapenda kuweka wazi shukrani zetu za dhati kwa Raphinha kwa juhudi na mchango wake alipokuwa nasi.

"Kila mtu Leeds United anapenda kumtakia Raphinha kila la kheri huko aendako na ni matumaini yetu atapata mafanikio makubwa Nou Camp na katika maisha yake yote."

Taarifa za kina kutoka vyanzo mbali mbali vya habari za michezo barani ulaya ni kwamba dili hilo lina thamani ya takriban €60m, huku Barcelona wakiwa wamezishinda Chelsea na Arsenal ambazo zote zilikuwa zikiwania saini ya mchezaji huyo wa miaka 25.

Post a Comment

0 Comments