Ticker

6/recent/ticker-posts

Barbara: Tumejipanga Tutarudi kwa kishindo 2022/23


Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa mkakati walio nao ni kurudisha mataji yote waliyopoteza msimu uliopita kutokana na maandalizi wanayoendelea nayo.

Barbara amesema malengo yetu ni kurudisha ubingwa wa ligi ya NBC, Azam Sports Federation Cup na kufika Nusu Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Barbara ameongeza kuwa msimu huu hatuna kuteleza tena tumejipanga ndani na nje uwanja na hakutakuwa na jambo lakuturudisha nyuma.

“Safari hii hakuna kuteleza tena, tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mataji yote kuanzia ligi kuu, FA na kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika,” amesema Barbara.


Post a Comment

0 Comments