Ticker

6/recent/ticker-posts

Aziz KI Kutua Yanga Muda Wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Aziz KI Kutua Yanga Muda wowote ASEC Mimosas wamuaga Rasmi

KLABU ya ASEC Mimosas kupitia Ukurasa wake wa Instagram Imempongeza na kumshukuru Mshambuliaji wake KI Stéphane Aziz kwa kumaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo aliyodumu nayo kwa misimu miwili na kufanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya Ivory Coast mara mbili. Tunakushukuru Aziz.

Wiki kadhaa zilizo pita viongozi wa klabu ya Yanga walionekana katika picha ya pamoja wakiwa na mchezaji huyo pamoja na meneja wake, taarifa za kina kutoka makao makuu ya klabu hiyo ni kwamba uongozi wa yanga umesha malizana na mshambuliaji huyo kilicho kuwa kinasubiliwa ni mkataba wake na ASEC Mimosas Uishe ili waweze kumtangaza.

Kuanzia sasa Stéphane Aziz KI atatangazwa kuwa mchezaji wa yanga baada ya klabu yake ya ASEC Mimosas kumpa mkono wa kwaheri.
Post a Comment

0 Comments