Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal : Wakamilisha Usajili wa Gabriel Jesus kutoka Manchester City

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Arsenal : Wakamilisha Usajili wa Gabriel Jesus kutoka Manchester City


Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mshambuliaji Gabriel Jesus kutoka Manchester City kwa kiasi cha pauni millioni 45, kwa mkataba ambao hitma yake sio bayana.

Ujio wa Jesus ndani ya Arsenal ni usajili wa nne wa kocha Mikel Arteta's, msimu huu, usajili wa wachezaji wengine ukiwa wa kiungo wa kati Fabio Vieira, mlinda mlango Matt Turner na mshambuliaji kutoka Brazil Marquinhos.

Arteta amesema “nimefurahishwa sana na ujio wa Jesus ndani ya Arsenal," huku akipongeza klabu hiyo kwa hatua hiyo nzuri.

Jesus atavaa jezi namba tisa Arsenal, ameondoka Manchester City baada ya kipindi cha mika tano na nusu.

Akiwa City, Jesus amechezea klabu hiyo mara 236, na kufunga mabao 95, na pia kusadia klabu hiyo kushinda mataji manne katika ligi kuu nchini Uingereza, mataji matatu ya kombe ya ligi pamoja na kombe la FA Cup.

Manchester City walimruhusu Jesus kuondoka baada ya kukamilisha Usajili wa mshambuliaji wa Norway, Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund kwa kiasi cha dolla millioni 51.2 mwezi  uliopita.


Post a Comment

0 Comments