Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal 2-0 Everton: Gabriel Jesus afunga tena katika ushindi mnono kujiandaa na msimu mpya

Mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Gabriel Jesus na Bukayo Saka yameipa Arsenal ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton wakijiandaa na msimu mpya mjini Baltimore siku ya Jumapili.

Kwa sasa timu hizo ziko ziarani nchini Marekani zikijiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya uingereza, katika mchezo huo takribani watazamaji  40,000 walifurika katika Uwanja wa Benki M&T kushuhudia mechi hiyo ya kirafiki.


Jesus alifungua ukurasa wa mabao baada ya nusu saa kwa kupachika bao la kwanza na dakika tatu baadae Mbrazil huyo akatoa pasi ya goli kwa Saka aliye ifungia Arsenal bao la pili.

The Gunners walianza mchezo huo kwa nguvu huku Jesus akilazimika kuokoa hatari kutoka kwa Jordan Pickford.

Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha wa Arsenal Mikel Arteta alisema kwamba alifurahishwa na matumizi ya wachezaji wake katika mazingira magumu.

"Vilikuwa vipindi viwili tofauti kabisa. Nadhani kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri sana, kilivutia sana, (sisi) tulielewa wapi nafasi zilipo na Umaliziaji ulikuwa mzuri sana," alisema.

"Tulikuwa tishio wakati wote na tulikuwa na mashambulizi mengi, mipira mirefu ilikuwa mingi, niliipenda sana,lakini kipindi cha pili tulianza kwa uzembe.

"Kwa ujumla vijana wanafanya kile wanachofanya mazoezini. Wamecheza vizuri sana, kwa kiwango cha juu  katika kila kipindi na unaweza kuona hilo kwa jinsi wanavyocheza."

Post a Comment

0 Comments