Ticker

6/recent/ticker-posts

Ángel Di María Kujiunga Juventus muda wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Ángel Di María Kujiunga Juventus muda wowoteJUVENTUS wamefika makubaliano na kiungo wa kimataifa wa Argentina Ángel Di María kujiunga nao kwa uhamisho huru. 

📑 Mkataba kati ya Juventus na Ángel Di María Inaandaliwa baada ya pande zote mbili kufikia mwafaka, Di María atasaini mkataba utakao mwezesha kuwepo Juventus kwa mwaka mmoja baada ya kila kitu kwenda vizuri .

🛩 Di María atasafiri kuelekea Italy mapema  wiki hii kukamilisha usajili wake, Huku Paul Pogba akitarajiwa kutua Turin siku ya jumamosi kukamilisha Usajili wake wa kujiunga na Juve akitokea Manchester United kama mchezaji huru.

🤝 Ángel Amekubali ofa ya Juventus licha ya  Barça na virabu vingine barani ulaya kuhitaji saini yake wiki kadhaa zilizo pita.

⛔️ Di María hakuwa tayari kurudi England licha ya kuwekewa ofa nzuri mezani, Alikuwa anahitaji kucheza nchi nyingine tofauti kabla ya kurejea kwao Argentina.

🤍 Kocha wa Juventus Allegri muda wowote atakuwa nao kikosini Paul Pogba na Di María Ambao wote wamejiunga kwa uhamisho huru,.


Post a Comment

0 Comments