Ticker

6/recent/ticker-posts

Andre Onana Atua Inter milan ya Italia

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Andre Onana Atua Inter milan ya Italia Akitokea Ajax Amsterderm ya Uholanzi

Klabu ya Inter Milan, imekamilisha usajili wa Goli kipa Andre Onana, kwa uhamisho huru kutoka kwa mabingwa wa Uholanzi Ajax Amsterderm.

Onana aliye na umri wa miaka 26 amesaini kandarasi ya miaka mitano ,ameletwa kuziba pengo la Samir Handanovic.

Onana amekuwa langoni katika klabu ya Ajax kwa miaka saba unusu akicheza michezo 214 .

Onana, ambae ni kipa namba moja wa Indomitable Lions anatarajiwa kuiwakilisha Cameroon katika fainali za kombe dunia nchini Qatar kati ya Novemba 21 na Disemba 18.

Nyota huyo anatarajiwa kuwa mchezaji wa nne kutoka Cameroon kucheza Inter Milan wakiwemo Pierre Wome, Daniel Maa Boumsong na Samuel Eto’o.


Post a Comment

0 Comments