Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Sc: Aishi Manula Afunguka Kuhusu kucheza Soka Nje

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Simba Sc: Aishi Manula Afunguka Kuhusu kucheza Soka NjeKipa namba moja wa Simba SC na Timu ya Taifa Taifa Star, Aishi Manula amesema ni kweli Watanzania wengi wanatamani aende kucheza soka nje  lakini changamoto ni kwamba hajapata timu anazozitaka.

Manula amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano wakati wa hafla za ugawaji tuzo za wachezaji usiku wa kuamkia leo.

"Wengi hawafahamu, wengi wanakwambia tu wanatamani kuona umeenda nje lakini bila kujali umeenda nje ya wapi, sisi makipa tuna mipaka, zile nchi za Kiarabu hasa wale Waarabu weupe hawawezi kuchukua Kipa kutoka nje ya nchi zao.

"Kwahiyo ili utoke Tanzania kuna nchi kadhaa tu ambazo umewekewa Congo, South Africa, Angola na kwengine ambayo leo hii Ligi yetu ya Tanzania ni kubwa, wote wanatamani kucheza Tanzania.

Soma Pia | Simba: Tunaanza kushusha wachezaji wapya

"Muda mwingine napata ofa, napata Timu wakati mwingine napata timu ambayo ni kubwa, ya average ambayo haishiriki michuano ya kimataifa lakini mimi lengo langu ni kushiriki michuano ya kimataifa ili nipate platfoarm zaidi.

"Muda mwingine natamani kwenda nje lakini nikiangalia nataka kucheza Champions league, Confederation cup kwahiyo kuna mambo mengi ambayo yananikabili ambayo Watanzania hawayaangalii wao wananitaka tu niende nje," amesema Manula.

Post a Comment

0 Comments