Ticker

6/recent/ticker-posts

NEEMA Yazidi Kuishukia Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Rais wa Young Africans SC Eng. Hersi Said na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Ndg. Tarimba Abbas wakionyesha makubaliano ya mkataba mpya kati ya SportPesa na Young Africans SC.

NEEMA yazidi kuishukia klabu ya Yanga ndivyo unavyo weza kusema baada ya jana kusaini dili nono la Sh 12 bilioni na Kampuni ya michezo ya bahati nasibu ya SportPesa.

Dili hilo jipya ni la miaka mitatu, hivyo linazidi kuifanya Yanga iogelee kwenye fedha na kama itakomaa tena kwenye michuano itakayoshiriki msimu ujao, itazidi kukusanya mkwanja wa maana kutoka kwa wadhamini waliopo klabuni hapo ikiwamo SportPesa na Kampuni ya Azam Media.

Mapema jana mchana Yanga, chini ya Rais Injinia Hersi Said ilisaini mkataba mpya na SportPesa baada ya ule wa awali wa miaka mitano kumalizika, huku dau likiwa limeongezeka maradufu.

Katika mkataba wa kwanza ambao SportPesa pia iliingia na Simba, klabu ya Yanga ilivuna kiasi cha Sh5.2 bilioni kwa miaka mitano, lakini kitendo cha kuchukua mataji matatu msimu uliopita yaani Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na ASFC, kimeipa mkwanja wa maana kutoka kwa wadhamini.

Mataji mawili tu ya Ligi Kuu na ASFC, Yanga imekomba Sh700 milioni kama bonasi kutoka kwa wadhamini wao wa Ligi Azam Media waliotoa Sh500 milioni, na NBC kutoa Sh100 milioni nas SportPesa kuwakabidhi jana Sh100 milioni.

Ukija kwenye ASFC, Yanga imelamba zawadi ya Sh 50 milioni za ubingwa, huku kwenye dili la Azam Media la kurusha maudhui, ikikomba Sh 2.4 bilioni na uhakika wa kupata bonasi ya Sh 4 bilioni kwa kuwa bingwa kwani mkataba huo wa miaka 10 wenye thamani ya Sh 41 bilioni unasema Yanga ikimaliza nafasi ya kwanza au ya pili basi itapata bonasi ya Sh 44.4 bilioni kwa miaka 10, ikiwa na maana kila msimu ikimaliza ndani ya nafasi hizo inabeba Sh4.4 bilioni.

Post a Comment

0 Comments