Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa
Mbeya ilivyozizima Yanga ikikabidhiwa Kombe la Ligi Kuu ya NBC
Hakika Ilikuwa ni shamrashara zilizoliteka Jiji la Mbeya baada ya klabu ya Yanga ya Dar es Salaam kutawaza mabingwa wapya wa Ligi Juu ya NBC msimu wa 2021/22.
Baada ya kukabidhiwa kombe hilo, wachezaji wa klabu ya Yanga SC walishangilia kwa mbwembwe hasa ikizingatiwa kuwa klabu hiyo ya Jangwani ilikaa miaka minne bila kutwaa taji hilo.
Shamrasha za kukabidhiwa taji hilo kwa mara ya 28 kwa 'Wananchi' zilifanyika katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya Jumamosi baada ya kukamilika mechi dhidi ya Mbeya City iliyoisha kwa sare ya 1-1.
Viongozi mbalimbali walishiriki tukio hilo wakiweno Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa.
Rais wa Shirikisho la Soka (TFF) Wallace Karia, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Mkurugenzi Mkuu wa NBC, Theobald Sabi.
Je, Unatafuta Ajira? Bofya hapa KutumaMaombi
0 Comments