Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za soka Barani Ulaya Jumanne

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Tetesi za soka Barani Ulaya Jumanne


Gabriel Jesus anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Arsenal kabla ya kununuliwa kwa pauni milioni 45 kutoka Manchester City.

Mshambulizi huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akisakwa na vilabu kadhaa, katika Ligi ya Premia na Ulaya, lakini akachagua kujiunga na The Gunners.

Jesus amecheza mechi 236 na kufunga mabao 95 akiwa na City tangu ahamie kutoka Palmeiras Januari 2017.

Ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu wakati akiwa Etihad Stadium, pamoja na Vikombe vitatu vya Ligi na Kombe la FA. Muda wake wa kucheza msimu ujao unaweza kuwa mdogo baada ya City kumsajili fowadi wa Norway Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund.

Tottenham inataka kumsajili mshambuliaji wa Brazil Richarlison 25, na winga wa Uingereza Anthony Gordon , 21 kutoka Everton katika mikataba miwili . Chelsea pia ina hamu ya kumsajili Richarlison.. (Sky Sports)

Lakini Everton haina hamu ya kumuuza Gordon ambaye kandarasi yake na klabu hiyo ya Goodison Park inakamilika 2025, ikiwa ni pamoja na kandarasi yoyote itakayomuhusisha Richarlison.. (Liverpool Echo)

Spurs pia wanapigiwa upatu kumsajili beki wa Barcelona na Ufaransa Clement Lenglet, licha ya Roma kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (London Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 18, atakuwa mchezaji anayesakwa sana na Real Madrid msimu ujao , licha ya kwamba klabu hiyo ya Uhispania inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea na Liverpool. (AS, via Mail)

Baada ya kufungua mazungumzo na klabu ya Manchester City kuhusu kumsajili Raheem Sterling ,27 Chelsea inajaribu kumsajili beki wa Uholanzi Frenkie de Jong 27 kutoka kwa mabingwa hao wa ligi ya kuu ya Premia.. (Telegraph )

Mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 30, anagtarajiwa kuondoka mwisho wa msimu wa 2022-23 akiwa mchezaji huru. Salah amefunga magoli 156 katika mechi 254 tangu alipojiunga na Reds mwaka 2017. (Mirror)

Arsenal wamewasilisha ofa ya pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Ajax Lisandro Martinez na wanaonekana kuiongoza Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 24. (Kioo)

Manchester United wanatumai kuhitimisha kandarasi za kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 30, na kisha wataelekeza umakini wao kumsaka mshambuliaji, huku Mbrazil wa Ajax Antony, 22, akiwa lengo lao kuu.

Mkataba wa kumnunua Antony umewekwa shakani huku Ajax sasa ikitaka pauni milioni 70 kumnunua fowadi huyo. (Kioo)

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi

Newcastle United wanatazamia kukamilisha usajili wa pauni milioni 32 wa mlinzi wa Lille Mholanzi Sven Botman, 22, lakini wako tayari kuendelea na harakati zao za kumnunua mshambuliaji wa Reims Mfaransa Hugo Ekitike, 20. (Mail).

Mfaransa Christophe Galtier, ambaye aliiongoza Nice msimu uliopita, anakaribia kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Paris St-Germain, huku Mauricio Pochettino akikaribia kuondoka katika klabu hiyo licha ya kushinda taji la ligi. (ESPN)

Barcelona hawataboresha ofa yao ya kandarasi kwa mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, ambaye mkataba wake na timu hiyo ya La Liga unamalizika tarehe 30 Juni. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia ana ofa kutoka kwa Bayern Munich, Chelsea na PSG. (Marca)

Dembele anatazamiwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake katika saa 72 zijazo. (Kioo)


Post a Comment

0 Comments