Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Yamrithisha Zoran Manojlovic Mikoba Ya Pablo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Simba Yamrithisha Zoran Manojlovic Mikoba Ya Pablo


Klabu ya Simba imemtangaza rasmi, Zoran Manojlovic raia wa Ureno kuwa ndiye kocha Mkuu wa timu hiyo kwa sasa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Zorana ambaye anakuja kurithi nafasi ya Mhispanola Franco Pablo anauzoefu mkuwa wa soka la Afrika, ambapo kwa mujibu wa Wikipedia Kazi yake ya mwisho ilikuwa kwenye klabu ya Al-Tai, ambapo hapo kabla pia alifundisha klabu ya CR Belouzdad, 

Pia kocha huyo anayesfika kwa soka la kushambulia kwa kasi na kujihami kwa pamoja, alizifudnisha klabu za Al-Hilal ya Sudani, Moghreb Tetouan, Wydad Casablanca ya Morocco pamoja na Sagrada ya Angola.

Mreno huyo anakuja kuifundisha Simba huku akiwa na jukumu la kukisuka upya kikosi cha mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu, pamoja na kuifanya timu hiyo kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika kwa msimu ujao.

Malengo mengine aliyopewa kocha huyo ni pamoja na kuipa timu hiyo ubingwa wa kombe la Azam Sports Federations kwa msimu ujao.

Kibarua cha kwanza cha Zoran kitakuwa ni katika mchezo wa Simba Day msimu ujao, ambapo mara baada ya hapo inatazamiwa atakutana na Yanga kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, endapo Yanga wakishinda kombe la shirikisho la Azam

Post a Comment

0 Comments