Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba SC Kusaka Mrithi Wa Tyron Damons

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu Simba Sc ipo kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya wa makipa baada ya Tyron Damons kupata dili jipya nchini Afrika Kusini.

Taarifa rasmi kutoka Simba imeeleza kuwa kwa hatua ambayo wamefikia wanamshukuru kocha huyo hivyo watasaka mbadala wake kwa ajili ya kuwa kwenye kikosi hicho.

 “Klabu ya Simba inamtakia kila la heri kocha wa magoli kipa Tyron Damons ambaye anataraji kuondoka klabuni kwetu mwishoni mwa msimu huu.

“Tyron amepata kazi kunako Klabu ya Orlando Pirates ya nchini kwao Afrika Kusini na tayari amewasilisha ombi la kutaka kuondoka klabuni kwetu na kujiunga na miamba hiyo ya Afrika Kusini.

“Tayari mchakato wa kutafuta mrithi wa Tyron umeanza na dhamira ni kumpata kocha mpya wa magoli kipa kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano,” imeeleza taarifa hiyo.

Mchezo wa mwisho kwa Simba msimu huu ni dhidi ya Mbeya Kwanza ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majimaji,Songea.

Kocha huyo alikuwa anawanoa Aishi Manula,Beno Kakolanya na Ally Salim kwa upande wa makipa wa Simba.

Post a Comment

0 Comments