Ticker

6/recent/ticker-posts

Shiza Ramadhan Kichuya Aweka Rekodi Ligi Kuu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Shiza Ramadhani Kichuya ni mchezaji wa kimataifa wa Tanzania wa Kandada, Kichuya aliitwa kwenye kikosi cha Tanzania kilichoshiriki michuano ya COSAFA 2017 na kufunga mabao mawili dhidi ya Malawi, Kwa sasa Staa huyo anasakata soka ndani ya Klabu ya Namungo.

Kichuya staa wa Namungo  amefunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi na kufanya aweze kufunga hat trick kwenye mchezo huo ikiwa ni ya pili ndani ya ligi.

Kichuya alifunga mabao hayo ilikuwa dk ya 23,50 kwa mkwaju wa penalti na lile la tatu ilikuwa dk ya 66 kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Soma Pia | Azam FC watasajili Namna Hii

Bao lingine la Namungo lilifungwa na Sixtus Sabilo dk ya 74, Mtibwa Sugar wao mabao yao yalifungwa na Nzigamasabo Stve dk ya 5 kwa mkwaju wa penalti na moja lilifungwa na George Makang’a dk ya 10.

Kwa msimu wa 2021/22 ni Jeremia Juma wa Tanzania Prisons alikuwa wa kwanza kufunga hat trick msimu huu ilikuwa mbele ya Namungo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Ni mzunguko wa 29 umeweza kumpata staa mwingine ambaye ameweza kufunga hat trick ndani ya ligi na wote wakiwa ni wazawa.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments