Ticker

6/recent/ticker-posts

Robert Lewandowski Kutua Barcelona

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

RAIS wa Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, Javier Tebas amekiri angependa kuidhinisha uhamisho wa Robert Lewandowski kuelekea FC Barcelona, lakini shughuli hiyo inategemea kama watakidhi 'vigezo' vya kiuchumi katika siku chache zijazo.

 


Rais wa Barcelona, Joan Laporta aliongoza mkutano wa wanachama wa Klabu hiyo wiki iliyopita ambapo alifichua mpango wa kurudisha nguvu za kiuchumi ambazo zitasaidia kupunguza upotevu wa kifedha ulitokea msimu wa 2021/22 na kuwawezesha kufanya usajili wa fedha nyingi msimu huu wa joto.


Mlengwa namba moja wa Barca bado ni Lewandowski, ambaye mwezi uliopita alisema hadharani kuwasihi Bayern Munich kumruhusu kuhamia Katalunya kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka ujao.


Tebas, mkosoaji anayejulikana wa shughuli za kifedha za Barcelona katika miaka michache iliyopita, amekiri kuwa angeidhinisha dili la Lewandowski ikiwa ni muhimu kwa klabu hiyo.


"Ninatumaini kwamba Lewandowski atachezea Barcelona na ana msimu mzuri. Ninatumaini kwamba, wale wawezeshaji wa kifedha ambao Laporta anawatumia watamfikisha Barcelona, ​​kwa sababu ni gwiji wa Bayern Munich na soka la Ulaya," alisema Tebas.


"Ikiwa kile walichokiidhinisha wanachama kitatekelezwa, ataweza kuichezea Barcelona. Kuna maslahi na kama watatekeleza hatua hizo wataweza kumsajili."

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments