Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester United Wamrejesha Donny van de Beek

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Manchester United Wamrejesha Donny van de Beek kwenye mazoezi kufuatia mkopo wake wa muda mfupi na Everton kufikia Kikomo.

Tangu ajiunge na Red Devils mnamo Agosti 2020 kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, amecheza mechi 50 kwenye mashindano yote.

Alitambulishwa kwenye kikosi na mkufunzi wa zamani wa United Ole Gunnar Solskjaer, lakini alishindwa haraka na kuhangaika kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

Soma Pia | Kocha Wa Manchester United Erik ten Hag Aanza Kazi Rasmi

Hivyo Basi Kama kawaida, alitolewa kwa mkopo kwa Everton mnamo Januari hadi mwisho wa msimu wa 2021-22.

Hata hivyo, kocha mpya Erik ten Hag amemhakikishia Van de Beek kwamba atakuwa na nafasi kwenye kikosi msimu ujao.

Wachezaji hao wawili wa Uholanzi walifurahia maisha pamoja wakiwa Ajax kabla ya kiungo huyo kwenda Old Trafford miaka miwili iliyopita.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments