Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester City Yanasa Saini Ya Kalvin Phillips Kwa Pauni 45M

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Manchester City, imefanikiwa kukamilisha dili la kumsajili kiungo wa Leeds United, Kalvin Phillips kwa pauni 45m.

Kiungo huyo mwenye miaka 26, katika hela yake hiyo ya usajili, pauni 42m ndiyo fedha iliyolipwa, huku pauni 3m itakuwa kwa ajili ya bonasi.

Mabingwa hao wa Premier League, wamemsajili Phillips kama mbadala wa Fernandinho ambaye alidumu kikosini hapo kwa miaka tisa kabla ya kuondoka mwisho wa msimu huu wa 2021/22.

 Phillips ambaye ni zao la Akademi ya Leeds, akiwa hapo amecheza mechi 214 tangu alipoanza kikosi cha kwanza mwaka 2015.

 Kiungo huyo anategemewa kuwa mbadala wa Rodri kwani Man City ilikuwa na kiungo mkabaji mmoja pekee baada ya kuondoka kwa Fernandinho.

Post a Comment

0 Comments