Ticker

6/recent/ticker-posts

Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel Atua Azam FC

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel Atua Azam FC

Baada ya juzi kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, matajiri hao wa Chamazi wameanza usajili kwa kushusha kiungo mshambuliaji raia wa Ivory Coast.

Kiungo huyo Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel (22) amesaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Sol FC ya nchini kwao.

Nyota huyo aliyekuwa kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), pia amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017-2018.

Kipre pia aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas msimu wa 2018-2020 na katika ukuaji wake alizichezea timu za taifa za vijana za Ivory Coast U-15 na U-17, pamoja na kikosi cha wachezaji wa ndani (CHAN) mwaka 2020.

Huo ni usajili wa kwanza kwa Azam kutangaza msimu huu huku ikieleza kuendelea kushusha vyuma vingine kwaajili ya msimu ujao.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments