Ticker

6/recent/ticker-posts

George Mpole Mfungaji Bora Ligi Kuu Tanzania Bara

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, George Mpole ameibuka kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2021/22.

Mpole ametwaa nafasi hiyo leo Juni 29, 2022 baada ya kufikisha mabao 17 kutokana na bao alilofunga katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kati ya Coastal Union na Geita uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani Tanga uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Bao hilo limemfanya Mpole ampiku Fiston Kalala Mayele wa Yanga mwenye mabao 16, ambaye leo hakufunga katika mchezo ambao Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.           
                    

Post a Comment

0 Comments