Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal Waongeza Dau Kwa Lisandro Martinez

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Arsenal Waongeza Dau Kwa Lisandro Martinez

ARSENAL imeboresha ofa yake kwa beki wa Ajax, Lisandro Martinez huku pia wakiwa wanatumaini kufikia makubaliano na Leeds United kuhusu Raphinha.

Arsenal imeboresha ofa yake na kufikia pauni milioni 34 kwa ajili ya Muargentina Martinez lakini Ajax wanataka kiasi kinachokaribia pauni milioni 43 huku pia Man United wakiwa wanamtaka.

Hata hivyo, United inahitaji kuuza kwanza kabla haijaanza mazungumzo juu ya nyota huyo mwenye miaka 24 anayeweza kucheza ulinzi wa kati, pembeni na kiungo mkabaji.

Arsenal imepanga kukutana na Leeds wiki hii wakijaribu kukamilisha usajili wa Raphinha kwa pauni milioni 50.

Arsenal wanataka kukamilisha usajili mapema ili kumsaidia kocha Mikel Arteta katika maandalizi.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments