Ticker

6/recent/ticker-posts

Aishi Manula Asaini Miaka Miwili Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Aishi Manula Ambaye ndiye mlinda goli katika klabu simba asaini kandarasi ya miaka miwili kuitumika klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi.

Kipa huyo wa kikosi cha Simba ambacho kwa sasa kipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola Aishi Manula ameongezewa mkataba wake wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo mkataba wake ulikuwa unakaribia kufikia ukingoni na kuna timu ambazo zilikuwa zimeanza mazungumzo naye kwa ajili ya kuinasa saini yake.

Manula ambaye ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa hajacheza kwenye mechi za ligi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia na nafasi yake ipo mikononi mwa kipa namba mbili, Beno Kakolanya.

Taarifa zimeeleza kuwa Manula ameongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo ambayo kwa sasa inafanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho Juni 29 wa ligi dhidi ya Mbeya Kwanza.

Manula msimu huu amecheza mechi 21 kafungwa mabao 11 na hajafungwa kwenye mechi 11baada ya kutumia dk 1,890

Post a Comment

0 Comments