Aug 23, 2013

Cheki hapa Interview ya Shilole Aliyofanya na VOA Washington DC

Read More

MAKAHABA WEMBAMBA WALIA BAADA YA KUKOSA SOKO SASA WAAMUA KUJIUZA KWA PROMOSHENI......!

MAKUBWA! Madogo yana nafuu! Wanawake wenye maumbile makubwa wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao jijini Dar, wamefunguka kwamba wanaume wamekuwa wakiwapenda kwa sababu ya ubonge wao.

Baadhi ya wanawake wenye maumbile makubwa wanaofanya biashara ya kuuza miili yao jijini Dar wanaodai kupendwa zaidi na wanaume.

Mijimama hiyo ilitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ikizungumza na Mwandishi wetu aliyekuwa katika oparesheni maalum ya kuhojiana nao ili kujua kinachowafanya wajihusishe na biashara hiyo inayohatarisha maisha yao.

Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Zainabu anayefanya biashara hiyo maeneo ya Sinza Afrika Sana, alisema umbo lake limekuwa likiwadatisha wanaume kibao.

“Kaka si unaiona hii shepu yangu, hapa kuna mwanaume anayeweza kunipita na kwenda kwa wale vimbaumbau,” alisema Zainabu huku akimuonesha paparazi wetu wasichana wembamba waliokuwa mbele yao.

Mwanamke mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Sara Mashauzi, aliyekuwa katika mawindo ya wanaume wakware na Zainabu alisema: “Mimi nilianza haya mambo baada ya kuachana na mume wangu, sasa kila ninakopita wanaume wakiniona tu huanza kunipigia miluzi na wengine kuniita, sista… sista… hongera…, nikaamua kujiuza ili nipate kipato kwani maisha yalibana sana.”

Sara aliongeza kuwa, wanaume wengi anaotoka nao wamekuwa wakimsifia kwa umbo lake ‘pana’ na kudai kwa siku huwa hakosi shilingi 50,000 na siku nyingine anapata hadi 80,000.

Karibu wanawake wote mabonge waliozungumza na paparazi wetu maeneo ya Kinondoni, Buguruni, Manzese na Oysterbay ambako biashara hiyo imeshamiri walidai maumbo yao yamekuwa yakipendwa sana na wanaume hususan waume za watu.

Mwandishi wetu alipomuuliza Sara, Zainabu na mwenzao aliyejitambulisha kwa jina la Sikitu kwamba hawaoni kama wanaharibu soko la wenzao wembamba, kama vile waliambiana jibu wakasema watajiju!

Baadhi ya madadapoa wembamba waliozungumza na mwandishi wetu, waliwafungukia majimama hao na kudai wamewaharibia soko lao na kusababisha wajiuze kwa promosheni.
Read More

SHAHIDI AGEUKA ‘BUBU’ KATIKA KESI YA WEMA


KESI inayomkabili staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao meneja wa hoteli, Goodluck Kayumbu ilizua kituko baada ya shahidi kugeuka ‘bubu’ ghafla.

Kituko hicho kilijiri Agosti 20, mwaka huu katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar ambako kesi hiyo inaunguruma.

Mmoja wa makarani wa mahakama hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema kitu kilichoonekana kituko ni pale shahidi wa mwisho aliposhindwa kutoa ushahidi baada ya sauti kukauka ghafla.

“Mlalamikaji alifika hapa na mashahidi wake watatu, Boniface Mati, Taito Osa na Melao ambapo wawili walitoa ushahidi lakini Taito alishindwa kutoa ushahidi wake kwani sauti ilikata ghafla na ndipo hakimu Bernice akamuamuru anyamaze na kupanga tarehe nyingine ya kuwasikiliza mashahidi hao,” alisema karani huyo.

Mlalamikaji wa kesi hiyo, alipoombwa na paparazi wetu azungumzie ‘ ishu’ ya shahidi wake kushindwa kuzungumza alisema amekubaliana na uamuzi wa mahakama na anasubiri tarehe ya kurudi mahakamani ambayo ni Septemba 30, mwaka huu.
Read More

RAY AMWAGIWA SIFA RUKUKI KWA KUKUZA VIPAJI

MWIGIZAJI Nyota na muongozaji bora wa filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ amemwagiwa sifa nyingi na mwigizaji wa kike Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ msanii huyo amedai kuwa Ray kupitia kampuni yake ya RJ Company ltd imekuwa ikiibua vipaji vipya kila siku na kutoa fursa kwa waigizaji chipukizi na kuigiza katika filamu zinazoandaliwa na kampuni hiyo.

Akihojiwa mwanadada huyo alisema kuwa Ray kutokana na umahiri wake wa uongozaji bora anatumia muda mwingi katika kukuza vipaji vya wasanii ambao hawajawahi kupata nafasi kabisa ya kuigiza na kunyimwa nafasi kabisa kwa wasanii wengine wenye majina katika tasnia ya filamu lakini hali kwa Ray ni tofauti.

“Sio siri nampenda sana Ray kwa juhudi zake anazofanya katika kuwachukua wasanii chipukizi ambao hawana kabisa connection na wasanii wakubwa, bila shaka ni ukweli usiofichika unapoanza katika uigizaji lazima ubebwe lakini kuna wasanii wengine hawana muda huo, Ray ni mfano wa kuigwa na anastahili pongeza sana kwa moyo wake,”anasema Batuli.

Batuli alitolia mfano kwa Miss Tanzania wa mwaka jana Salha Isael na kuwa mwigizaji kinara katika filamu ya Bad Luck kitu ambacho kwa watayarishaji wengine isingekuwa rahisi kumwamini msanii mpya, sifa anazopewa Ray kiukwelia anastahili kwani mtayarishaji huyu amekuwa mbele sana katika kutoa mchango wake katika harakati za ukuzaji wa filamu Bongo. 
 
BIG UP RAY KWA JUHUDI ZAKO
Read More

CRAZY GK ANAJIANDAA KURUDI RASMI KWENYE GAME

Mwanzilishi wa kundi la East Coast Team (ECT) “Crazy Gk” aliyetamba na nyimbo kama sauti ya Manka, miko kumi ya rap, sister sister na simba wa afrika anamipango ya kurudi kwenye game la bongo flava.

Msanii huyo aliyepotea kwa muda mwingi akiwa masomoni sasa anataka kurudi tena kwenye game na atazindua wimbo wake mpya wiki ijayo kupitia radio station tofauti tofauti hapa Tz.
Read More

BWANA MISOSI FT DULAYO ~ TUNGI NA MISOSI (OFFICIAL VIDEO)

Read More

BODI YA UKAGUZI YAIPIGA STOP FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU

Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo, filamu hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City inahitaji marekebisho.

Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumika katika waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.

Hivi sasa baada ya urasimishaji wa filamu mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya filamu zimekuwa makini na kuhakikisha kuwa filamu zinazoingia sokoni na zile zinazozinduliwa kukaguliwa kabla ya kufanyika kwa matukio hayo kama ilivyokuwa awali, kama filamu hiyo ya Foolish age itashindwa vigezo vya madaraja yanayotolewa na Bodi hiyo haitaonyeshwa.

Lulu ndio mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2013 kupitia tamasha la filamu la kimataifa la ZIFF katika kipengere cha tuzo za Bongo movie kilichopewa jina la Zuku Bongo movie Awards zilizotolewa katika ukumbi wa Ngome Kongwe.
Read More

BATULI.....WADADA WENGI WA BONGO MOVIE TUNAPENDA KUCHUKULIANA MABWANA

MWIGIZAJI wa kike wa filamu Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefunguka kwa kuongelea ugomvi na chuki ambazo zimekuwa zikiripoti kwa akina dada kutoka Bongo movie sababu kubwa ni ugomvi wa kuibiana wanaume mapedeshee ambao wamekuwa wakiwaweka mjini kwa kuwapangia majumba na kuwapatia magari wakitanua nayo mjini.

“Chuki yetu wasanii wa Bongo movie ni kuchukuliana mabwana yaani mtu ukiwa na mtu anayekusaidia huwezi kabisa kumtambulisha kwa shoga yako kwani ukimpa mgongo tu si wako huyo tena, naongea bila uoga tunahitaji maisha mazuri lakini filamu hazilipi hivyo ukiona msanii wa kike anafanya kitu lazima ujue nyuma yake kuna mtu na si kwa ajili ya malipo ya filamu ni mapedeshee hao,”anasema Batuli.

Lakini pia Batuli anawalaumu sana wasanii wenzake wa kike kwa kukosa ubunifu na kutotumia fursa wanazopata kutoka sehemu mbalimbali hata serikali pia, msanii huyo amedai kuwa kuna msanii aliwahi hata kupata mwariko kwa rais wa nchi nyingine lakini kutokana na uwezo wake wa kutokufiri hakwenda kuonana na rais, hivyo Batuli anasisitiza kuwa hakuna msanii wa kike anayeweza kusimama kama yeye zaidi ya kuwategemea mapedeshee waliojificha nyuma yao.
Read More

DIAMOND APATA DEMU MPYA

MWANAMUZIKI Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amegeuka gumzo nchini Kenya baada ya mrembo mmoja aliyejipatia jina kupitia Runinga ya KTN, Angel Maggy kutangaza penzi lao upya kwa mara nyingine.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari za burudani vya Kenya, mara baada ya Diamond kufanya shoo mbili katika Miji ya Nairobi na Mombasa nchini humo, alipogeuza kisogo kurejea Bongo ndipo ukaibuka mlipuko wa habari zilizomhusu na mrembo huyo.

Ukiachilia mbali gumzo la vurugu zilizotokea baada ya Diamond kucheleweshwa kupanda stejini na kusababisha watu kupigwa chupa huko Mombasa, kilichofuata ni skendo ya mapenzi na mrembo aliyepata jina kupitia kipindi cha Tujuane cha KTN.

Habari hizo zilieleza kuwa mara tu baada ya kutua nchini humo, Diamond alipokelewa kwa bashasha na mrembo huyo akiwa na wenzake wanne.

Ilielezwa kuwa tofauti na warembo wengine, Angel alimganda Diamond kila kona kuanzia akiwa jijini Nairobi katika shoo yake ya kwanza na siku ya pili aliambatana naye hadi Mombasa kwenye shoo ya pili.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' akiwa naAngel.

Ilisemekana kuwa alipokuwa akifanya shoo kwenye Ukumbi wa KICC, Nairobi siku ya kwanza, Diamond aliimba wimbo wake wa Ukimuona maalum (dedication) kwa ajili ya Angel, jambo lililomfanya mrembo huyo kuonekana ‘spesho’ miongoni mwa maelfu waliohudhuria onesho hilo.

Imeripotiwa kuwa baada ya shoo hiyo kumalizika ‘naiti’ kali, Angel alionekana ‘beneti’ na Diamond wakielekea katika hoteli aliyofikia staa huyo Nairobi.

Hata hivyo, hakuna mahali palipoelezwa kama walilala wote usiku huo.

Habari zilizidi kutonya kuwa kesho yake mrembo huyo alionekana kila kona aliyokatiza Diamond mjini na baadaye kwenye shoo ya Mombasa ambako huko ndiko kulipotawaliwa na vituko vya kufa mtu.

Ilidaiwa kuwa kwenye shoo hiyo ndiko Angel alipokuwa akiahidi kumpa Diamond mahaba mazito kupitiliza yale aliyokuwa akipewa na zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu kwa kuwa wanamjua.

Ikasemekana kuwa wakati Mkenya huyo akitamba kwa mara nyingine kuwa ndiye demu wa Diamond na kupewa jina hilo (Demu wa Diamond), warembo wenzake walikuwa wakimuonea wivu kwa kuwa mwanamuziki huyo ni gumzo kwa wanawake nchini humo.

Ilidaiwa kuwa wakati Angel akijitapa kuwa ndiye malkia mbele ya mfalme Diamond, mashosti zake waliojiita mashemeji, nao walikiri kumkubali mwanamuziki huyo.

Ilisemekana kuwa Angel na wenzake walimbatiza Diamond jina la Mfalme wa Afrika Mashariki hasa alipofanya shoo iliyowaacha watu hoi kwa namna alivyokonga nyoyo zao.

Baada ya shoo kuliibuka madai mazito kuwa Angel alipata nafasi adimu ya kwenda kulala na Diamond katika hoteli aliyofikia huko Mombasa Beach.

Iliendelea kufahamika kuwa wawili hao hawakuonesha ugeni wa kuonana kwani walionekana ni watu waliozoeana kwani mara kadhaa Angel wa Diamond alinukuliwa akisema yeye ndiye malkia wa staa huyo wa Wimbo wa Kesho.

“Wanaonekana kuzoeana kwa sababu mwaka jana walikutana Mombasa ‘so’ siyo mara yao ya kwanza, wanakumbushia, sema tu safari hii imekuwa ‘too much’,” ilisomeka sehemu ya habari hiyo.

Katika kuonesha kuwa kuna kitu kati ya wawili hao, Angel amejichora ‘tattoo’ ya jina la Diamond na alama za ‘malavu’ kwenye mkono wa kushoto huku rafiki zake wakidai kuwa ana nyingine ya mwanamuziki huyo aliyojichora sehemu nyeti.

Baada ya kuwepo kwa habari hizo ambazo hakuna mahali Diamond alipopewa nafasi ili kupata mzani wake, gazeti hili lilimtafuta Diamond na kumpa A-Z ambapo alikiri kumfahamu Angel na kufunguka anachokijua.

“Namjua (anatajiwa Angel), kila nikienda huko huwa anapenda kuwa na mimi. Nilipofika kule (Nairobi) niliandaliwa mamodo ambao nilikwenda nao Mombasa na huyo mrembo alikuwa mmoja wao.

“Alinionesha hata hiyo tattoo akaniambia ananipenda sana na ndiyo maana kajichora jina langu.

“Kweli kuna picha tulipiga, huwa huyo mrembo anajitangazia huko Kenya kuwa anatoka na mimi kimapenzi ila si kweli namjua tu kawaida,” alisema Diamond kwa makubaliano kuwa akimaliza shoo ya Fiesta leo mkoani Tabora atatafuta chansi kulizungumzia sula hilo kwa kina.

Hata hivyo Penny alipotafutwa kupitia simu ya kuganjani hakupatikana hewani lakini kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu, mrembo huyo hajui chochote kinachoendelea.

Septemba mwaka jana,kunataarifa zilienea baada ya Angel kujitapa kulala na staa huyo alipokwenda nchini humo kwa ziara ya shoo ambapo Diamond alisikitishwa na kitendo hicho hivyo habari hii ni mwendelezo wa madai ya mrembo huyo kuwa penzi lao limeibuka upya.

Via:GPL
Read More

HUYU NDIYE MSANII ALIYEFILISIKA KUTOKANA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

WIMBI la uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya limeshika kasi hivi sasa kwa wasanii na watu mbalimbali huku Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe akilivalia njuga kulikomesha.

Wakati hayo yakiendelea, mnenguaji aliyetikisa anga la muziki wa dansi nchini, Aisha Mohammed Mbegu ‘Aisha Madinda’ amejuta kutokana na kufilisika baada ya kutumia madawa ya kulevya.

Akizungumza katika mahojiano maalum hivi karibuni, Aisha alisema alipokuwa juu kwa unenguaji alifanikiwa kumiliki mali mbalimbali zikiwemo nyumba tatu pamoja na gari lakini madawa yamemlostisha.

Akisimulia jinsi nyumba zake tatu zilivyopotea, Aisha alisema alianza kuweka rehani ‘bondi’ nyumba yake ya Kigamboni akiwa anachukua fedha kidogokidogo hadi alipoambiwa fedha zake zimekwisha.

“Baada ya kuiweka bondi nyumba ya Kigamboni na kuambiwa sina changu nikaenda kuuza nyumba ya Kimara mwisho,” alisema.

Baada ya kumaliza nyumba zake, mnenguaji huyo akadai kuwa aligeukia gari lake aina ya Toyota Mark II ambalo nalo aliliuza.

“Niliona ujinga nilikuwa nikipata tabu ya kutafuta fedha za kununulia unga wakati gari nilikuwa nalo, nikaisukumia mbali,” aliongeza huku akisikitika kwa uamuzi huo ambao sasa anaujutia.

Aidha, Aisha alisema hivi sasa anawachukia wanaouza madawa ya kulevya kwa kuwa wanatajirika wakati wao kama watumiaji wanafilisika kifedha na kuumia kiafya.

“Sisi wanunuzi tunakuwa na maisha magumu wakati wenzetu wanatajirika, binafsi sikuwahi kutegemea kama ningeishi maisha kama haya, nawashauri mastaa wengine wanaondelea kutumia madawa hayo waache mara moja kwani madhara yake ni makubwa kiuchumi na kiafya,” alimalizia mnenguaji huyo ambaye hivi sasa yuko fiti na anaweza kupanda jukwaani wakati wowote.
Read More

WATANZANIA 3 WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI HUKO SOUTH AFRICA KISA DAWA ZA KULEVYA

Watanzania watatu wameuawa hivi karibuni jijini Cape Town, Afrika ya Kusini kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Watanzania hao walipigwa risasi na kundi la watu waliokuwa wameficha nyuso zao nje ya duka lijulikano kama Maisha Tuck Shop jumanne iliyopita katika barabara ya Veld, Athlone, Cape Town.

 
Watanzania wawili walifariki papo hapo na mmoja kufia hosipitali. Mtu mwingine, raia wa Afrika Kusini, alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo. Mmiliki wa duka la Maisha Tuck, Ashim Nassoro, alisema kuwa aliona kundi la watu wakiwa na bunduki za aina ya AK-47 na pistols wakipiga risasi nje ya duka lake.

Bw. Nassoro alidai waliouawa walikuwa marafiki zake, alisema yeye alikuwa nyumbani na mke wake na mtoto wake, ambapo ni karibu na duka hilo aliposikia milio ya risasi.

 
 “Nilikuwa ndani na nilimwambia mke na mtoto wangu walale chini mpaka milio ya risasi iishe” alisema Nassoro na kuongeza “waliwapiga risasi watu waliokuwa ndani ya nyumba halafu wakaenda kwenye duka. Walipiga risasi watu wawili dukani, mmoja aliyekuwa kwenye geti na mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye nyumba.”

Nasroro aliongeza kuwa alikuwa anawajuwa Watanzania hao kwa sababu wote wanatoka Tanzania na wamekuwa wakiishi pamoja tokea walipowasili Cape Town miaka mitano iliyopita. Mtu mwingine aliyeshughudia tukio hilo alisema kuwa waliowauwa Watanzania hao walikuwa hawana wasiwasi na walirudi kwenye gari yao taratibu na kuondoka eneo la tukio.Kufuatia tukio hilo, polisi ilimkamata Abdus Salaam Ebrahim ambaye ni kiongozi wa kikundi kinachopiga vita dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya nchini humo kinachojulikana kama People Against Gangsterism and Drugs (Pagad). Abdus Salaam Ebrahim amefikishwa mahakami leo kwa mashtaka ya mauaji.

Hata hivyo, mahakama imeyaondoa mashtaka hayo kwa muda kufuatia ombi la mwendesha mashtaka ili kuruhusu uchunguzi zaidi kufanyika. Wakati hakimu akiyandoa mashtaka hayo, wafuasi wa kikundi hicho cha Pagad waliokuwa wamejazana mahakamani hapo walishangilia huku wakisema “Allahu Akbar”. Majina ya Watanzania waliouawa hayakuwekwa kwenye charge sheet.

Pagad ni kikundi kilichoanziswa mwaka 1995 kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya kwenye jiji la Cape Town baada baada ya juhudi za serikali kulegalega. Kampeni ya kikundi hiki ilianza mwaka 1996 baada kumkamata, kumpiga na kumchoma moto hadi kufa Rashaad Staggie ambaye alikuwa kiongozi wa kikundi cha uhalifu jijini Cape Town. Serikali ya Afrika Kusini ilishawahi kudai huko nyuma kuwa Pagad ni kikundi cha kigaidi baada ya kudaiwa kulipua kwa bomu hoteli ya Planet Hollywood mwaka 1998. Hata hivyo, Pagad ilipinga kuhusika kwenye shambulio hilo.

Kikundi hiki kilipotea lakini kikaja kuibuka tena kuanzia mwaka 2011 na kampeni yake ya kuchukua mitaa inayotawaliwa na uhalifu na biashara ya madawa ya kulevya. Wadadisi wa mambo wanadai kuwa kurudi tena kwa Pagad kwa gia ya kupambana na uhalifu, hasa madawa ya kulevya, itafanya hali kuwa mbaya hasa kwenye jimbo la Western Cape.

Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la milipuko ya mabomu kwenye sehemu zinazouza magari na pia kwenye nyumba za makazi ya watu zilizopo Athlone na maeneo mengine jijini Cape Town. Matukio haya yamekuwa yakitokea zaidi kwenye nyuma za makazi zinazotuhumiwa kutumika kufanyia biashara ya madawa ya kulevya. Kikundi cha Pagad kimekanusha kujihusisha na matukio hayo.
Read More

HIKI NDIO KINACHOENDELEA HUKO KURASINI BAADA YA BOMOA BOMOA KUPITA

Read More