Mar 7, 2013

HII NDIYO HALI YA HOSTELI PALE UDSM


Inasikitisha sana na kuhuzunisha kuona watoto wa wakulima wanaotafuta shahada ya elimu ya juu (university) ndani ya chuo bora kabisa Tanzania na Africa kwa ujumla.Je:
1.ni uzembe wa serikali ya chama cha mapinduzi?
2.ni uzembe wa uongozi wa chuo kikuu cha dar es salaam?
3.ni uzembe wa wanafunzi wenyewe wanaoshindwa kufanya kazi za ziada wakiwa vyuo vikuu na kupata hela zinazoweza kuwafanya wakapanga nje ya vyuo ambao wanaweza kupata malazi yenye mazingira bora zaidi ya haya?
4.kwa mazingira kama haya wanafunzi wanapata usingizi wa kutosha ili waweze kuweka vichwa vyao katika hali nzuri ya kuhudhuria na kuelewa lecture za siku inayofuata?
5.watanzania wanafahamu kuwa wanachuo kikuu wanalala katika mazingira kama haya yenye joto kali kama hili la jiji la dar es salaam bila hata feni wakitokwa jasho mwili mzima usiku kucha?
6.viongozi wa serikali wanayafahamu mahasibu haya?
7.wanafunzi wa chuo kikuu na uongozi wa chuo kikuu cha UDSM wameridhika na mazingira haya ya malazi?

Opinion
Ni aibu kwa kwa serikali,chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM) na wasomi wote waliopo na waliowahi kupitia chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM)

Post a Comment